Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amekitembelea Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amekielekeza Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) mkoani Morogoro kusaidia taifa kutokana na miradi mbalimbali ambayo mataifa ya nje yanakuja kuwekeza nchini kupitia Biashara ya Kaboni.

Amesema NCMC itumie wataalamu wake kwa kadili inavyoweza kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujikita zaidi kwenye biashara hii, sababu wanapokuwa na elimu ya kutosha katika Biashara ya Kaboni ambayo sasa imekuwa ikiangaliwa zaidi kwa kuongeza maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla itasaidia pia katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Waziri Masauni ameyasema hayo Februari 5, 2025 mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya Mafunzo kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Biashara ya Kaboni na Shughuli za Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC).

“Imani yangu kupitia kituo hiki tutaifaidisha taifa katika maeneo mawili, kwanza kwenye fursa ambazo zinaweza kutupatia fedha taifa pamoja na kusaidia kuratibu miradi itakayopunguza gesi joto katika dunia,”

“Uratibu wa Biashara ya Kaboni chanzo chake kikubwa ni mabadiliko ya tabianchi ambayo yanasababisha na hewa ya kaboni kutokana na shughuli mbalimbali za uchumi na athari za mabadiliko ya tabianchi hata kama Afrika mchango wake sio mkubwa lakini athari zake zinatukumba,” amesema Waziri Masauni.

Ameongeza kuwa leo hii tumeshuhudia vyanzo vya maji vikikauka na sekta nyingi zikiathirika kama vile kilimo, maji, nishati pamoja na fukwe kuathirika ambapo maji huingia katika makazi ya watu.

      

Related Posts