Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Ashatu Kijaji amekutana na Bw. Jules Kortenhorst, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bridge Carbon ya nchini Marekani ambayo imewekeza Tanzania kwenye miradi ya Kaboni kupitia nishati safi ya kupikia na “Nature Based Solution”. Mheshimiwa Waziri ameipongea Kampuni hiyo kwa uwekezaji wake na pia alimuhahakikishia Bw. Jules kuwa Tanzania, imejipanga kuweka mazingira wezeshi Kwa wawekezaji ili kukuza biashara Kaboni na pia itaendelea kumpa ushirikiano .
Aidha, Bw. Jules aliishukuru Tanzania na ameahidi kuwekeza zaidi kwenye nishati safi ya kupikia ili kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa wingi nchini Tanzania. Mkutano huo umefanyika tarehe 15 Novemba, 2024 pembezoni mwa Mkutano wa COP29 Jijini Baku, Azerbaijani.