4.-(1) Taasisi yoyote inayotekeleza mradi wa kaboni au mtu yeyote anayetekeleza mamlaka chini ya Kanuni hizi atazingatia misingi ya-
(a) maendeleo endelevu;
(b) utunzaji endelevu wa mazingira
(c) uwazi;
(d) ufanisi;
(e) msingi wa kulipia uchafuzi wa mazingira;
(f) ujumuishaji wa masuala ya kijamii na kiuchumi na manufaa mapana ya kimazingira; na
(g) viwango vya kimataifa.
(2) Mtu yeyote anayetekeleza mamlaka kwa mujibu wa Kanuni hizi, wakati wa kutoa uamuzi wowote, amri yoyote, utekelezaji wa mamlaka yoyote au utendaji wa jukumu lolote atapaswa kuongozwa na masharti ya kanuni ndogo ya (1) pamoja na msingi wa usawa, haki, wajibu na majukumu ya pamoja lakini yanayotofautiana kulingana na mazingira ya kitaifa.