Kamati ya Bunge yaipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ubunifu mkubwa unaobeba uhalisia katika utekelezaji wa majukumu yake.

Pongezi hizo zimetolewa leo Machi 18, 2025 Bungeni Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2024/2025 na makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2025/2026.

Dkt. Mhagama amesema Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa ofisi ya mfano kwa sasa kutokana na kufanya kazi nzuri kutokana na watendaji wake kutekeleza maelekezo mbalimbali ya kamati na hivyo kuwezeka kupata matokeo makubwa katika kipindi kifupi.

“Wajumbe wa kamati hii tupo kwa zaidi ya miaka 10 sasa, lakini kwa kifupi hiki kifupi tumeshuhudia mageuzi makubwa ya kiutendaji katika utekelezaji wa majukumu ya ofisi hii, tunaomba tuendelee kushirikiana ili kufikia malengo” amesema Mhe. Mhagama.

Ameongeza kuwa watendaji wa ofisi hiyo wamekuwa wakisivu katika kupokea ushauri, maoni na maelekezo ya kamati kuhusu masuala mbalimbali yanayojadili ndani ya kamati na bunge kwa ujumla na hivyo kusaidia mhimili wa Bunge kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Amefafanua kuwa kamati hiyo itaendelea kutoa ushirikiano na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia hoja mbalimbali zinazowasilishwa ndani ya Bunge ili kuhakikisha mihimili hiyo inafanya kazi katika kuwasaidia wananchi.

Amesema kuwa katika kipindi cha nyuma kulikuwepo na changamoto mbalimbali ingawa kwa sasa hali hiyo imebadilika kutokana na viongozi waliopo kuwa wasikivu na wenye kuzingatia maelekezo na hivyo kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameishukuru kamati hiyo kwa ushiriakiano inaoendelea kuipatia ofisi hiyo na hivyo pongezi hizo zitakuwa chachu ya kufanya kazi nzuri zaidi.

Hii ni kamati kubwa sana, kupokea pongezi hizi si jambo jepesi….hii inatupa faraja kuwa tunachokifanya kinaonekana na tunaahidi kuongeza juhudi katika kutekeleza maelekezo mbalimbali yanayotolewa” amesema Mhe. Masauni.

Aidha Mhe. Masauni amesema Ofisi hiyo itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia ushauri na maoni ya kamati hiyo ili kufikia malengo iliyojiwekea.

Related Posts